Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Nimeumia kuondoka Niyonzima, sina jinsi- Msuva

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amefunguka kuwa, kitendo cha Haruna Niyonzima kuondoka kikosini hapo, kimemuachia maswali mengi yasiyokuwa na majibu, hivyo ataendelea kummisi kila kukicha.
Niyonzima ambaye msimu ujao ataitumikia Simba, ameondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba huku akishindwa kuongeza kutokana na kushindwana kimaslahi na viongozi wake hao wa zamani.
Akizungumza na Championi Ijumaa,Msuva alisema, kati ya wachezaji wote wa kigeni aliowahi kucheza nao ndani ya Yanga, Niyonzima ndiye aliyetokea kuendana naye kwa kila kitu.
“Kwa kweli Haruna nilimzoea kupitiliza, alikuwa kama mtani wangu, hivyo basi kwa hali hiyo iliyotokea, kwa upande wangu nimeumia sana lakini sina jinsi.
“Kuondoka kwake haimaanishi kwamba nitashuka kiuwezo, bali nitaendelea kupambana na nitashirikiana na wengine kama nilivyokuwa nashirikiana naye.“Nitamisi vitu vingi kutoka kwake, najua hata yeye huko alipo nadhani anafahamu ameniacha kwenye hali gani, nasema hivyo kwa sababu kati ya wachezaji wa nje niliowahi kucheza nao, yeye pekee ndiye nimevutiwa naye,” alisema Msuva.
Ibrahim Mussa