Ray: Embu niangalieni vizuri mtapata jibu
Msanii wa Filamu Bongo, Ray Kigosi ameendelea kusistiza kuwa weupe wake
unatokana na kunywa maji mengi na kufanya mazoezi na si kujichubua kama
wengi wanavyodhani.
Kupitia mtandao wa instagram Ray ameandika haya na kuweka hiyo picha
hapo juu. “Kuna wakati mwingine ukikaa kimya unaweza ukaufanya uongo
ukawa ukweli.. swali langu ni moja kwenu nyie mnaosema najichubua hivi
ni kweli mnamjua mtu anayejichubua?,” amehoji Ray na kuendelea.
“Embu niangalieni vizuri mtapata jibu, tatizo letu sisi Watanzania
tunapenda sana kuaminini uongo kuliko ukweli. Nilishawaambia ukitaka
kuwa na ngozi yenye nuru kama yangu fanya sana mazoezi kunywa sana maji,
hiyo ndio dawa mbona hata madoctor wanalijua ilo,” amemaliza kwa
kuandika.