USAJIRI ULAYA:ZIDANE AZUNGUMZA NA MBAPPE
Zinedine Zidane ameshazungumza na Kylian Mbappe katika harakati zake
za awali kumshawishi Mfaransa huyo kutua Real Madrid, kwa mujibu wa L'Equipe .
kwa ajili ya mchezaji huyo mahiri wa Monaco lakini Real Madrid wapo
kwenye nafasi nzuri zaidi kumsajili kwani Florentino Perez anahitaji
saini yake.
SPURS YAVUTIWA NA SUSO
Tottenham wanavutiwa kumsajili kiungo wa AC Milan Suso, Kwa mujibu wa Marca .
Milan bado hawajamfunga kinda huyo wa zamani wa Liverpool kwa mkataba
mpya San Siro, na Mauricio Pochettino anataka kuhakikisha mchezaji
huyo anatua London katika jitihada za kuunda kikosi thabiti cha
ushindani Ligi ya Mabingwa.