Nemanja Matic Akaribia kutua Man United!
Kwa mujibu wa habari Matic ameshafikia makubaliano binafsi na United, ofa tu ndiyo inayosubiriwa kuwasilishwa Chelsea
Chelsea inakaribia kumsajili Bakayoko kutoka Monaco jambo ambalo litaacha mlango wazi kwa Nemanja Matic kuondoka darajani.
Tangu kuondoka kwa Jose Mourinho kiungo Nemanja Matic amekuwa
haaminiwi na kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte na hajapewa nafasi
ya kutosha kushuka dimbani.
Lakini Mourinho bado anamuhitaji Nemanja Matic ili acheze na Paul
Pogba katika kiungo cha Manchester United usajili ambao unasemwa kila
siku katika vyombo vya habari na sasa umekaribia kutimia.
Taarifa zinasema Manchester United na kiungo huyo tayari wameshafikia
makubaliano binafsi na sasa kinachosubiriwa ni kwa Chelsea kupokea ofa
kutoka kwa United.
Mawasiliano kati ya kocha Jose Mourinho na kiungo huyo wa Serbia
yanaonekana ni mazuri bado na wapo karibu, hii inaweza kuwa nafasi kwa
Mourinho mwenyewe kufanya ushawishi wa kumnunua Matic.
Matic anahitajika United kwenda kushirikiana na Paul Pogba
anayeonekana kuelemewa na majukumu mengi katikati ya uwanja huku
msaidizi wake bora ambae ni Michael Carrick umri ukielekea ukingoni.