Header Ads

PropellerAds

Breaking News

TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA NA CONTE KUONDOKA CHELSEA?


Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekerwa na klabu hiyo kutokubali kufanya usajili dirisha la uhamisho wa majira ya joto na anaweza kuondoka klabuni hapo kwa mujibu wa Sky Sport Italia .
Conte, ambaye aliondoka Juventus kwa sababu ya mazingira kama hayo, anataka wachezaji maalumu kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini anaona miamba hao wa London hawana mpango wa kuingia sokoni.

Bosi wa zamani wa Borussia Dortmund ametajwa kuwa mrithi wake.

REAL YAIZIDI PSG KUMFUKUZIA DONNARUMMA


Real Madrid wanaongoza katika mbio za kumsaini Gianluigi Donnarumma kutoka AC Milan, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa  Sky Sport Italia .

MADRID WANATAKA £78M KWA AJILI YA MORATA


Real Madrid wametangaza kuwa bei ya Alvaro Morata ni paundi milioni 78 ikiwa Manchester United wanataka kweli kumsajili mshambuliaji huyo, kwa mujibu wa  The Independent .
United walikuwa wakitarajia watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo kwa kiasi cha paundi milioni 60, lakini rais wa klabu Florentino Perez amesema kwa bei hiyo mchezaji huyo hatoki.

JUVE WAKATAA OFA YA ARSENAL KWA CUADRADO


Dau la Arsenal la paundi milioni 17 kwa ajili ya winga wa Juventus Juan Cuadrado limekataliwa na mabingwa hao wa Serie A, kwa mujibu wa The Sun .

Arsene Wenger anataka kujiandaa kwa maisha bila ya Alexis Sanchez kwenye kikosi chake na anaamini Cuadrado angeziba vema pengo la mchezaji huyo anayetaka kuondoka Emirates.

Juventus wamesisitiza kuwa bila ya ofa ya paundi milioni 30 hawawezi kushawishika kumuuza mchezaji wao.

ARSENAL YAMTENGEA DAU KJAER


Arsenal imetoa dau la euro milioni 12 kwa ajili ya mchezaji wa Fenerbahce Simon Kjaer, kwa mujibu wa  TurksVoetbal .

Miamba hao wa Emirates watakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan ingawa klabu hiyo ya Uturuki haipo tayari kupokea fedha chini ya €15m.

ARSENAL YAMFUKUZIA SMALLING


Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazofuatilia maendeleo ya beki wa Manchester United, Chris Smalling kwa mujibu wa  The Sun .

Mashetani Wekundu wakiwa katika harakati za kumsajili Victor Lindelof, wanaweza kumwachilia Muingereza huyo majira ya joto, West Ham nao wanataka kumsajili.

CHELSEA WANAMTAKA CABALLERO


Chelsea wanataka kumsajili kipa wa zamani wa Manchester City Willy Caballero kushirikiana na Thibaut Courtois, Mwandishi wa Argentina Cesar Luis Merlo amekiambia  TyC Sports .

Caballero amehusishwa na tetesi za kutaka kujiunga na Newcastle baada ya kuondoka City, lakini bosi wa Chelsea Antonio Conte anamtaka kuziba pengo la Asmir Begovic, aliyejiunga na Bournemouth.

BARKLEY HURU KUONDOKA EVERTON


Everton wapo tayari kumruhusu Ross Barkley kuondoka klabuni hapo majira ya joto baada ya kukataa fursa ya kuwa mchezaji anayepokea mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo, kwa mujibu wa   Mirror .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekataa dili la £100,000 kwa wiki katika Goodison Park, na sasa Ronaldo Koeman anataka kusajli wachezaji wawili kuziba pengo lake.