Boss wa Chelsea Abramovich azuia usajili wa Bonucci
Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amemzuia Kocha wa Antonio Conte kumsajili beki kutoka Juventus, Leonardo Bonucci.
Taarifa zilizokuwapo ni kwamba Kocha Conte ana mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia ambaye wamekuwa naye karibu kwa kipindi cha miaka miwili.
Beki huyo wa Jeventus anatajwa kuondoka kwenye klabu yake katika dirisha la usajili msimu huu na kocha wake Massimiliano Allegri yupo tayari kumuachia kutokana na kushindwa kuonyesha makali msimu ulioisha.
Hata hivyo, zuio hilo linatokana na mkakati wa klabu ya Chelsea kusajili wachezaji chipukizi wasiozidi umri wa miaka 30.
Bonucci mwenye miaka 33, anapaswa kuangalia klabu nyingine kwani kinachoonekana umri umekuwa kikwazo kwake.
Mabingwa Chelsea wa England bado wanafikiria zaidi kusajili beki ikiwa ni mojawapo ya eneo ambalo wamepanga kuboresha msimu ujao.