MAKALA: Kula Chipsi mara 2 au 3 kwa wiki kunasababisha vifo kwa vijana
Utafiti uliofanywa na Wanasayansi kutoka National Research Council umegundua
kuwa ulaji wa chipsi au viazi vilivyokaangwa mara mbili au zaidi kwa
wiki husababisha vifo vya mapema kwa vijana kwa zaidi ya 70%.
Akielezea
utafiti huo Dr. Nicola Veronese amesema ulaji wa viazi hauleti tatizo
lolote la kiafya bali vinapokaangwa ndipo hupelekea kiwango kikubwa cha
kolestro kunyonywa na mishipa ya damu pindi mtu anapokula hivyo
kusababisha ugonjwa wa cardiovascular.
Katika
utafiti huu watu 4,440 walihusishwa na walikula chipsi mara tatu kwa
wiki kwa muda wa miaka minane ambapo zaidi ya watu 236 walifariki
kutokana na ugonjwa wa cardiovascular kuliko magonjwa mengine.
Aidha,
wa mujibu wa utafiti huo, imebainika kwamba ukiacha matatizo kama unene
kupita kiasi na ugonjwa wa kisukari,ulaji wa chipsi umetajwa kuwa
hatari zaidi kwa kusababisha magonjwa yanayopelekea vifo vya haraka.