Alhaj Mzee Yusuph afunguka kilichosababisha kuacha muziki
Aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuph ambaye kwa sasa anafahamika kama Alhaj Mzee Yusuph amefunguka kuhusu kuacha kwake muziki na kufanya toba ili kurudi kuwa muumini na kutoa daa’wa.
Akizungumza kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo June 15, 2017 Alhaj Mzee Yusuph
amegusia pia jinsi maneno ya watu yalivyofuata baada ya kutangaza na
hatimaye kuacha kabisa muziki huku akielezea namna alivyokuwa anakataza
watu kwenye Kundi lake wasitende maovu.
“Mimi
nimeacha muziki kwa sababu nataka kuwa Muumuni wa Dini ya Kiislamu na
kumfuata Mtume Muhammad (SAW). Nilipopata nafasi ya kwenda kuhiji Makka
na kushika Al Kaaba nilimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu".
“Nilipoanza kubadilika
nilikuwa nakataza pombe kwenye Band yangu. Siku nisiyowepo walikuwa
wanasema Simba leo hayupo. Nilipokuwa nakataza haya mambo wengi walikuwa
wakiniambia kwa nini nisifungue Madrasa. Kubadilika kwangu niliachana
kwanza na starehe magoma kwanza maana ilikuwa ni kama kunywa maji tu
unaposikia kiu.
“Nilizungumza
mimi na Mungu wangu nikisema: ‘Wewe ndiye mwenye kutoa msamaha’.
Nikafanya show ya mwisho Dodoma nikaachana na muziki. Nilimwambia kwanza
mke wangu mdogo mimi nimeacha muziki. Kesho yake nikamuambia mke wangu
mkubwa nimeachana na mziki, hawakuamini.” – Alhaj Mzee Yusuph.