ROMA KAJITOLEA KUFUNDISHA SOMO LA HISABATI
MKALI wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ anatarajiwa kuwa mwalimu wa muda wa somo la hisabati leo (Juni 15) katika Shule ya Msingi, Mchikichini iliyopo Mbagala-Kibondemaji jijini Dar.
Akizungumza na Showbiz Xtra , Roma anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Viva R.O.M.A Viva, K, Ivan na Kaa Tayari alisema kuwa, ameamua kuchukua nafasi hiyo kwanza kujikumbushia kazi yake ya ualimu aliyokuwa akiifanya zamani ambapo alikuwa mwalimu mzuri wa somo la hisabati.
“Somo la hisabati ni miongoni mwa masomo yanayotengwa sana na wanafunzi wengi hivyo basi nikiwa kama mwalimu niliyepitia kufundisha somo hili, nimeona vyema kuhamasisha wanafunzi walipende na kuliamini. “Nitagawa vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba na pia kuwafundisha somo hilo. Kila mmoja nitahakikisha amehamasika na somo hili na kulipenda kama masomo mengine,” alisema R.O.M.A.
Kesho kufutuRisha Mbali na R.O.M.A kutembelea shule hiyo ya Mchikichiki, kesho (Juni 16) mkali huyo ataelekea katika Kituo cha Watoto Yatima cha Nira ambapo atatoa msaada sambamba na kufuturisha.
Shoo ya Dar Live sasa Naye Meneja na Mratibu wa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, Juma Mbizo alisema baada ya R.O.M.A kufanya yote hayo ya kijamii, mashabiki wake wote waliommis jukwaani watarajie shoo ya nguvu katika Sikukuu ya Idd Mosi.
“Shoo itatambulika kama Nishushe Dar Live ambapo Roma akiwa na wasanii kibao wakiongozwa na Mr. Blue wataliamsha dude ndani ya Dar Live na kugonga nyimbo zake zote zinazobamba. “Nikukumbushe tu mara ya mwisho kwa R.O.M.A kupiga shoo ya kihistoria ilikuwa mwaka jana katika Mkesha wa Mwaka Mpya ambapo alipanda jukwaa moja na mkali, Darassa na kuzoa kijiji. sasa safari hii jibu utatoa mwenyewe akishuka
jukwaani,” alisema Mbizo.
WENGINE SASA
Mbizo aliongeza listi kuwa mbali na Mr.Blue na R.O.M.A mashabiki wategemee jukwaa kufunikwa na wakali wa Hip Hop kama Darassa na Stamina huku Snura akiwarushia vyura jukwaani.
Shoo ya watoto nayo ndani Mbizo aliongeza kuwa, mbali na shoo hizo pia pazia la burudani litafunguliwa Sikukuu ya Idd Mosi mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa kundi la sarakasi lisilo na mpinzani Bongo, Wakali Dancers pamoja na wakali wa nyimbo za Asili, Makhirikhiri kutoka Tanzania ambao wataliamsha kwa kutoa burudani kwa watoto.
“Kutakuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea, kucheza ndani ya ndege na mingine mingi.
“Katika kunogesha burudani kwa watoto, kwa mara ya kwanza mkali wa vichekesho anayebamba katika Kipindi cha Ze Comedy, Bambo atakuwepo kuvunja mbavu za watoto wote watakaojitokeza huku akigawa zawadi ndogondogo kwa watakaotoka chicha.
Zanzibar Stars kuibuka Baada ya kupotea kwa muda, kundi kongwe la Muziki wa Mwambao, Zanzibar Stars linatarajiwa kuibuka kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live likiwa na vichwa hatari kama Bi. Mwanahawa, Sabaha Mchacho, Jokha Kassim, Mosi Suleiman, Ally Jay, Zubeda Mlamali na wengine kibao. Mtonyo sasa! Mbizo alimaliza kwa kutaja kiingilio kwa siku hiyo kuwa, burudani kwa wakubwa itakayoanza saa 2:OO usiku itakwenda kwa shilingi 7,000 huku watoto ikiwa shilingi 3,000 tu!