Header Ads

PropellerAds

Breaking News

TETESI ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA MAY 31/2017

BEKI wa Mbao FC, Mghana Asante Kwasi, ameipiga chini ofa ya klabu ya Singida United inayofundishwa na kocha Hans van der Pluijm, iliyotaka kumsajili kwa ajili ya kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, badala yake amesema angependa kujiunga na Azam FC.
Akizungumza jana, Kwasi alisema ana amini Azam FC ni klabu sahihi kwake kujiunga nayo kutokana na kuvutiwa na namna inavyoendeshwa. Alisema kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kumalizika, alifuatwa na wadau wa klabu ya Singida United wakimshawishi ajiunge nao lakini aliwagomea akitaka apewe muda wa kutafakari wapi ni mahali sahihi kwake kutimkia.
“Kuna timu nyingi Tanzania lakini navutiwa zaidi na Azam jinsi inavyojiendesha, ni klabu inayofanya mambo yake kisasa sana. “Kuna meneja wangu yupo Afrika Kusini yeye ndio ana jukumu la kunitafutia timu, unajua lengo langu ni kucheza timu itakayonifanya nionekane, hii ndiyo sababu iliyonifanya niipotezee Singida United.
Kipa mkongwe wa Yanga, Ally Mustapha 'Barthez' na beki wa pembeni wa timu hiyo, Oscar Joshua ni kati ya wachezaji watakaokuwepo kwenye kikosi cha Singida United katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Kama hawatakuwa katika kikosi hicho basi safari yao kwa upande wa Yanga itakuwa imeishia hapo. Barthez na Joshua ni kati ya wachezaji ambao hawakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina katika msimu uliopita wa ligi kuu.
Wachezaji hao wote bado wana mikataba ya mwaka mmoja wa kuichezea Yanga kwenye msimu ujao wa ligi. Kwa mujibu wa taarifa za ndani wachezaji hao wataondolewa Yanga na kupelekwa Singida inayofundishwa na Kocha Mkuu Mholanzi, Hans Pluijm aliyekuwa anaifundisha timu hiyo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na George Lwandamina.
Mtoa taarifa huyo alisema, wachezaji hao walikuwepo kwenye orodha ya wachezaji watakaochwa katika msimu ujao, lakini kutokana na mikataba yao kutomalizika watapelekwa kwa mkopo.
"Barthez na Joshua hawana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Lwandamina na pia hana mipango nao, hivyo kama uongozi tumeona tuwatoa kwa mkopo.
"Tutawatoa baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Singida na kukubali kuwachukua, hivyo tumeona tuwaachie waende huko wakacheze,"alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Barthez kuzungumzia hilo alisema kuwa ":Bado sijapata taarifa rasmi ya kupelekwa kwa mkopo, ni tetesi ninazozisikia pekee kama ulivyosikia wewe ni vema tukasubiria kwanza kabla ya mimi kuongea chochote.
"Kingine ni ngumu mimi kuondoka kabla ya kupelekwa huko na Yanga, kama unavyojua bado nina mkataba wa kuichezea Yanga,"alosema Barthez.