Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Steve Nyerere afunguka haya kuhusu Mama Wema Sepetu

Steve Nyerere
Muigizaji mkongwe wa Filamu Tanzania Steve Nyerere kati ya mambo aliyozungumza ni kuhusu kuyaweka pembeni mambo yote yaliyotokea baina yake na Mama yake Wema Sepetu.
Steve Nyerere amesema katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ameamua kusamehe na kusahau kila kilichotokea baina yao na lazima waanze upya kwa sababu hata Vitabu vya Dini vinaeleza.
“…lazima tusamehe ili kuanza mwanzo. Kwa hiyo, mimi nasema kwanza vile vitu vilipita – yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Yule ni Mama – ni Mama yangu, ni rafiki yangu, ni ndugu yangu, ni mwanafamilia. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
“Mzazi haombi samahani; mzazi hakosei. Mzazi anapatia lakini mwenyewe ndani ya nafsi yake anasema pale nilimkwaza mwanangu au pale nilimkosea mwanangu. Naamini ndani ya nafsi yake anasema hapa nilimkwaza mwanangu au hapa nilimkosea mwanangu.” – Steve Nyerere.