Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Hatma ya Wenger ndani ya Arsenal imetangazwa leo:


Baada ya kutokuwa na mwenendo mzuri kwa club ya Arsenal katika kipindi cha hivi karibuni, kuliibuka mjadala katika mitandao ya kijamii kuhusiana na mashabiki wa timu hiyo wengi kushinikiza afukuzwe, hususani baada ya kukosa nafasi ya kushiriki Champions League.
Arsenal itakosa kushiriki Champions League msimu wa 2017/2018 kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki katika michuano hiyo kwa miaka 20 mfululizo, hivyo kutokana na kushuka huko wengi walikuwa wanahisi Wenger atafukuzwa. Leo May 31 2017 uongozi wa club ya Arsenal umethibitisha kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili. 
 Wenger atadumu ndani ya Arsenal hadi mwaka 2019, maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka Wenger aipe Arsenal Ubingwa wa 13 wa FA kwa kuifunga Chelsea na kuifanya kuwa club pekee iliyotwaa taji hilo mara nyingi zaidi ikifuatiwa na Man United mara 13.