Header Ads

PropellerAds

Breaking News

IBRAHIM AJIB ATIMIZA AHADI YAKE KWA AZIZI

Ibrahim Ajibu

Kuelekea Fainali ya FA dhidi ya Mbao FC.Ibrahim Ajib akutana na Azizi 'Mtoto wa Ajib' na kula nae chakula cha mchana. Pamoja na kula chakula cha mchana na mtoto Azizi pamoja na Mama yake Mzazi ,Ajib alimzawadia zawadi mbalimbali zikiwemo Begi la shule, madaftari, Jezi mpya ya Simba, soksi pamoja na vifaa vingine vya shule na mazoezi.
'Nimefurahi sana Leo kukutana na Baba yangu Ajib, nilitamani sana kumuona na kumshika mkono. Ahsante sana Baba Ajib kwa zawadi zako hizi nzuri. Nitaendelea kusoma na kifanya mazoezi kwa bidii ili nifike hatua uliyopo wewe pamoja na Mbwana Samatta ' Ni maneno ya Azizi' Mtoto wa Ajib' kwenda kwa Ajib wakati alipokuwa akiondoka.
Ajib ameahidi kuendelea kushirikiana na familia ya mtoto Azizi katika mambo mbalimbali ili kumwezesha kukuza kipaji chake na kufikia ndoto zake.