Header Ads

PropellerAds

Breaking News

RIPOTI KUHUSU AJALI YA MELI KUWAKA MOTO ZANZIBAR DESEMBA 15

Hii stori imenifikia baada ya kuenea kwenye mitandao pamoja na picha zikionesha tukio la meli kuwaka moto Nimeipata ripoti pia kwenye habari ya ITV kwamba meli hiyo ya MV Royal imepata ajali ya kuwaka moto ikiwa katikati ya safari kutoka Unguja kwenda Pemba, moto huo umeunguza injini za meli hiyo lakini kwa bahati nzuri ikatokea meli nyingine ya MV Serengeti, ambapo ikafanyika kazi ya kuokoa abiria waliokuwa kwenye meli hiyo pamoja na kuuzima moto huo.
Kamanda wa Polisi Pemba, Shehan Mohamed Shehan amesema meli ilikuwa na abiria zaidi ya 300 pamoja na watoto 70.. wote wametoka salama na meli imefanikiwa kuvutwa mpaka bandarini Pemba. Sauti yenye stori yote kutoka ITV hii hapa, pole kwa watu wetu wote waliopata msukosuko kwenye ajali hii.