Header Ads

PropellerAds

Breaking News

HATIMAE RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI.SOMA ZAIDI!!!!!

Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanz ania, Dr John Magufuli anatangaz a baraz a la mawaz iri wa Jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanz ania. Tuwe pamo ja kulifahamu baraz a letu. Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza. Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani. WIZARA Ofisi ya Rais, Tamisemi, utumishi na utawala bora: Mawaziri ni George Simbachawene na Angela Kairuki, Naibu waziri Jaffo Selemani Said Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Makamba na naibu wake ni Mpina Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma Ulemavu: Waziri ni Anthony Mavunde Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, Wiliam Nashe naibu waziri Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Kijachi Nishati na madini: Waziri ni Professa Muhongo, Naibu waziri ni Medadi Katiba na sheria: Waziri Harisson Mwakyembe Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Waziri ni Augustino Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba. Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Mwinyi Wizara ya mambo ya ndani: Charles Kitwamba Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage Elimu, Sayansi na ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya Afya, maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Hamis Andrea Kingwangala Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Kamwene Swali: Tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata Umesema kukutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi? Niliyowachagua wote wana CCM na walinadi ya sera hapa kazi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili. Manyerere Jackton: Kwa kupunguza baraza la mawaziri, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani? Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34. Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu, wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua,Uhai Production: Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharesha zile hela? Magufuli: Swali hilo jibu analo kamishna wa kodi TRA Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi? Jibu: Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba?