Header Ads

PropellerAds

Breaking News

SOMA KWA MAPANA KWANINI MHE.DK.JOHN MAGUFULI ALIVYO ONDOA SHEREHE ZA UHURU

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ameagiza siku ya sikukuu ya Uhuru, 9 December hakutakua na sherehe za kitaifa na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.

Maamuzi haya yamekuja siku chache baada ya Dk.Magufuli kutoa tena agizo la fedha zaidi ya milioni 250 ambazo zilikuwa zitumike kwenye sherehe za ufunguzi wa Bunge, Dodoma kuelekezwa kwenye ununuzi wa vitanda vya wagonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais amechukua maamuzi hayo kutokana na kukerwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao tayari umepoteza maisha ya watu na bado umeendea kukumba maeneo mbalimbali nchini.

Kwa niaba ya Rais, Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue baada ya kufanya ziara katika hospitali ya muhimbili alisema Rais ameagiza kuwa siku hiyo hakutakuwa na sherehe zozote za kitaifa na badala yake wananchi wataitumia kufanya usafi katika maeneo yao.

“Rais amesema suala la kuwepo ugonjwa Kipindupindu halikubaliki, jambo hili limemkera sana, tunasherehekea miaka 54 ya uhuru lakini bado kipindupindu kinatusumbua sana, amesema kama Watanzania lazima tulishughulikie, haiwezekani akija mgeni kama Obama tunafanya usafi lakini akiondoka tunaendelea kuwa wachafu, ameamua tarehe 9 December siku ya uhuru hakutakuwa na sherehe yoyote badala yake watu wakasafishe maeneo yao”..Ombeni Sefue.Chanzo cha habari millardayo.com