Manchester City yasajili kipa kwa rekodi ya dunia
Timu ya Manchester City imefikia
makubaliano ya kumsajili kipa Ederson Moraes, toka klabu ya Benfica ya
Ureno na kuwa usajili wa pili wa Man City baada ya ligi kumalizika.
Uhamisho
wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 umeigharimu City kitita cha paundi
milioni 35 na kumfanya kuwa kipa wa pili ghali katika historia baada ya
Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus akitokea Parma mwaka 2001.
City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili kumnasa kiungo Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.