Header Ads

PropellerAds

Breaking News

RIYAD MAHREZ KUONDOKA LEICESTER CITY

Kiungo wa Leicester City Riyad Mahrez amesema kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye miaka 26 aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Le Havre ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paundi 400,000 mwaka 2014, amesema alikubali kubaki klabuni hapo kwa msimu mwingine baada ya majadiliano mazuri na mwenyekiti walipoishangaza dunia kwa kuwa mabingwa wa EPL msimu uliopita.
Riyad Mahrez
Lakini kwa sasa amesema kuwa tiyari amekwisha iambia klabu juu ya kuondoka kwake na anaomba wamruhusu kufanya hivyo.Mahrez mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa England mwaka 2016, amecheza mara 48 msimu huu akifunga magoli 10 na kutoa pasi saba za magoli. Leicester ilianza msimu wa ligi ya England vibaya na hatimaye kumaliza katika nafasi ya 12, lakini ikafika hatua ya robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.