Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Lizer amtaja msanii wa WCB anayefurahia kufanya naye kazi

Mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Wasafi Records, Lizer amemtaja msanii wa WCB ambaye anafurahi zaidi akiwa anafanya naye kazi.

Lizer amesema anafurahia kufanya kazi na Raymond kwa kuwa ni msanii ambaye aliibua kipaji chake. “Msanii yoyote anayejua mimi nina enjoy sana kufanya naye kazi, ukimuelekeza fuata hiki anafuata lakini naweza kusema kwa kuwa Raymond ndiye msanii aliyegundua kitu kilichopo ndani ya Lizer huwa nina enjoy naye zaidi kwasababu ndiye msanii ambaye nilitoka naye.” Amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, ya Njombe, Gami Dee.
Hata hivyo Lizer alisema alijifunza production kipindi anafanya muziki baada ya kuona watayarishaji ni wasumbufu sana ndipo hapo akaamua kufanya kitu hicho ili ajifanyie kazi zake japo kwa sasa hafikirii kuimba tena kama zamani.
Imeandikwa na: Gami Dee (Ice Fm) Instagram: @gamideetz Phone: 0715971027