Header Ads

PropellerAds

Breaking News

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI PROFESA MAJIMAREFU HOSPITALI ANAKOPATIWA MATIBABU


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.

Akiwa hospitalini hapo Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha. Kwa upande wake Profesa Majimarefu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali hospitalini hapo pamoja na viongozi wengine kwani amedai kuwa hali hiyo inamfariji kwa kiasi kikubwa. “Nawashukuru viongozi wenzangu wote waliofika kunitembelea tangu nimelazwa hospitalini hapa, lakini Pia naishukuru Serikali kwa kunipa kibali cha kurudi India kwa ajili ya matibabu zaidi kwenye hospitali ya kwanza iliyonifanyia upasuaji wa mguu”. Alisema Maji Marefu.