Header Ads

PropellerAds

Breaking News

WAFANYABIASHARA WATAMANI KUJIINGIZA KWENYE UMACHINGA


WAFANYABIASHARA nchini wametishia kuacha kazi hiyo rasmi na kufanya shughuli za kimachinga kama Serikali haitatenga haraka maeneo ya wafanyabiashara wadogo kwa kuwa wanapata hasara kwa kukosa biashara huku wakilipa kodi.
Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Rais John Magufuli kuamuru wamachinga wasibughudhiwe, waachwe wafanye biashara zao katika maeneo ya mijini.
Akizungumza jana Dar es Salaam , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja alisema wafanyabiashara wenye maduka wanaweza kuingia katika mfumo huo ili kuepuka kodi.

“Wafanyabiashara wanaweza kuacha shughuli hiyo rasmi na kuwa wamachinga, kwa sababu wanatambua kwamba hawatawajibika kulipa kodi ya Serikali,” alisema Minja.
Aidha, aliitaka Serikali kuchukulia suala hilo kwa uzito, kwa kuwa wafanyabiashara wanatumia mashine za elektroniki (EFDs) ambao wanatakiwa kuonesha mauzo yao na kuangaliwa wasiendelee kupata hasara kutokana na wamachinga kwani kunafanya wasipate wateja na hivyo kukosa faida.,br/> Minja aliongeza kuwa wafanyabiashara wengi wanaofanya shughuli za kibiashara kihalali wangependa kutumia njia isiyo rasmi kama ya wamachinga, kwa kuwa kuna mteremko fulani wa kutolipa kodi ambao unawafanya wapate faida zaidi. Alisema kuruhusu wamachinga kufanya shughuli zao karibu na maduka si sahihi, kwani alibainisha kwamba wanatakiwa kutengewa maeneo ambayo yao ambayo watakutana na wateja wao.
Minjua alisema anaamini kuna wateja wa wamachinga, wa madukani na wa maduka makubwa, hivyo mteja wa wamachinga hatarajii kuona mteja wao akienda kununua mahitaji yake dukani.
Aliitaka Serikali kufanya utekelezaji wa haraka kutenga maeneo ya wamachinga ili kila mfanyabiashara aweze kuwa eneo ambalo atakutana na kuhudumia wateja wake.