Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Jose Mourinho anataka kukutana na Ed Woodward kujadili orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili msimu wa majira ya joto

Zlatan Ibrahimovic (Mchezaji huru)
Zlatan Ibrahimovic anapatikana kwa uhamisho wa bure, ni moja ya wachezaji ambao Jose Mourinho anawataka Manchester United kuongeza magoli na kuwapa uzoefu washambuliaji chipukizi. Mswidi huyo atatua Old Trafford kwa mkataba wa mwaka mmoja na atakuwa mchezaji sahihi kumpa Marcus Rashford darasa.
Eric Bailly (Villarreal)


Jina Bailly limekuja kuwashangaza mashabiki wengi wa United, mchezaji huyo raia wa Ivory Coast anaweza kukidhi haja za Jose Mourinho kama beki wa kati. Itakuwa ni kama kamari kumchezesha mchezaji mdogo kama yeye asiyekuwa na uzoefu wa kutosha pamoja na Chris Smalling hata hivyo.Alisha tua tayari kwa Euro million E30.
John Stones (Everton)


Mourinho alipambana kwa kucha na meno kumleta Stones Chelsea msimu uliopita lakini hakufanikiwa. Ni dhahiri Mreno huyo atarudi tena kumsaka beki huyo wa Kiingereza majira ya joto.
Miralem Pjanic (Roma)


Mourinho atahitaji kuimarisha safu ya ulinzi baada ya Morgan Schneiderlin na Bastian Schweinsteiger kushindwa kuwika msimu uliopita. Dau la kumtoa Pjanic Roma ni paundi milioni 35 tu na rais wa Roma amekiri kuwa raia huyo wa Bosnia anaweza kuondoka iwapo dau hilo litafikiwa.
Andre Gomes (Valencia)


Juventus wanamtaka Gomes lakini kulingana na ukweli kwamba kiungo huyo ni Mreno na wakala wake ndiye Yule wa Mourinho, uwezekano mkubwa atatua Manchester United. Gomes ametamka hadharani kuwa Mourinho ni Kocha bora.
James Rodriguez (Real Madrid)


Mcolombia huyo ameshindwa kumvutia Zinedine Zidane katika Real Madrid na hali akiwa si moja ya wachezaji wenye tabia anazopenda Mourinho, Upatikanaji wake wa haraka unaweza kuilazimisha United kumsajili mapema.
Paul Pogba (Juventus)


Pogba ni moja ya wachezaji hatari sana Ulaya kwa sasa ambao karibu kila timu ya ligi za Ulaya inatamani kuipata saini yake. Kutokuwepo kwa Man United kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kunawapa nafasi ndogo sana kumrejesha kiungo huyo Old Trafford.
Raphael Varane (Real Madrid)


Mourinho alimleta Varane Real Madrid na ana mahusiano mazuri na mchezaji huyo. Mfaransa huyo anasugulishwa kibenchi na Pepe pale Bernabeu na huenda akafungua mlango kutua Old Trafford kuungana na Mourinho.
Nemanja Matic (Chelsea)


United wameripotiwa kuanza kuwasiliana na kiungo huyo wa Chelsea ambaye alikuwa jiwe la pembeni katika kikosi cha Mourinho kilichotwaa taji 2015. Mourinho ni dhahiri atapenda kuungana na kiungo wake huyu wa zamani.
Joao Mario (Sporting Lisbon)


Kiungo mshambuliaji wa Ureno amekuwa lulu baada ya kung’ara msimu uliopita akiwa na Sporting lakini Mourinho atalazimika kutoa kitita cha euro milioni 45 kumnunua mchezaji huyo.