Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Kama una safari ya kwenda Dodoma inabidi uongeze umakini barabarani.. (Picha)

Najua kuna watu huenda wako njiani au wana mipango ya kusafiri kwenye mji ambao una headlines za vikao vya Bunge kwa sasa, Dodoma town.. au wengine wana safari kwenda mikoa mingine kupitia mkoa huo.
Naomba nikufahamishe kwamba kuna sababu za kuwa na umakini wa ziada unapokuwa barabarani, kama unatumia barabara ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa kuna uharibifu umetokea na kama mvua ikiendelea kupiga kabla ukarabati haujafanyika basi hali huenda ikawa mbaya zaidi. Mvua imenyesha na kumetokea uharibifu wa baadhi ya sehemu, pengine inapita gari moja tu yani haziwezi kupishana mbili kwa wakati mmoja.
Kwa mbali wanaonekana mafundi wakifanya ukarabati sehemu ya barabara iliyoharibika, hapo upande mmoja wa barabara pekeake ndio unaopitika
Chanzo cha habari Millardayo.com