Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Waziri mkuu wa Tanzania Aamuru watumishi Hawa kutiwa Mikononi mwa polisi Mara moja.

Ni headlines ndani ya kazi ya Rais mpya kwenye awamu ya tano ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ambaye kila siku amekuwa kwenye headlines kwa kukata bajeti na kupunguza matumizi ya serikali kwenye vitu kadhaa. Sasa leo November 27 2015 aliyezichukua headlines ni Waziri mkuu aliyemteua wiki iliyopita Dodoma, waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa wote wa mamlaka ya mapato (TRA) waliohusika na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta ubadhirifu mkubwa. Maafisa hao watano ambao kwa sasa majina yao yamehifadhiwa ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za kusafiria ambapo hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo yapo kwenye kumbukumbu za mamlaka ya Bandari lakini katika mtandao wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) hayaonekani. Habari kamili inaandaliwa kutoka Ikulu na itapanda very soon hapa millardayo.com lakini kwa sasa anza na hizi picha zikimuonyesha Waziri mkuu kwenye hiyo ziara ya ghafla bandarini.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa TRA na TPA.Chanzo cha Habari Millardayo.com