Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Shindano la watu wabaya lamalizika mshindi anyakua Dola 500 za Marekani.


Kama vile ambavyo kuna mashindano ya watu wenye sura nzuri, mvuto, warembo, na mashindano mengine yote tuliyozoea, kuna mashindano ya wenye sura mbaya pia toka Zimbabwe.
Jamaa anaitwa Maison Sere, hana kibarua chochote rasmi kinachomuweka mjini lakini kagusa kwenye stage inayohusu mashindano ya watu wenye sura mbaya na kaibuka na ushindi wa dola 500 mkononi kama utani yani !!

                        Washiriki wengine wa shindano hilo wakiwa kwenye stage.
Unaambiwa kwenye mashindano hayo, William Masvinu ni jamaa ambaye amewahi kushinda Taji hilo mara tatu mfululizo amelalamika kwamba kumefanyika upendeleo ndio maana safari hii amelikosa taji hilo na kujikuta akishika nafasi ya pili, anachoamini ni kwamba kwa ubaya wa sura yake anastahili #1.
 Maison Sere kwenye pozi lake.

Maison Sere hana meno kadhaa mdomoni, na amefanikiwa kuibuka na ushindi huo kwa kuwashinda washiriki wengine watano huku akijikunjia na mkwanja wake dola 500 ambazo ukizichenji zinagusa kama Milioni 1 hivi !!
Stori yake imegusa vichwa vya habari vya Kimataifa pia, unaweza kucheki ripoti yake kutoka kituo cha TV ya China CCTV.Chanzo Millard ayo.com