Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Alikiba afunguka “Kuna wasanii walimtafuta Producer kutaka material ya nyimbo zake”


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Kiba alimaarufu Alikiba amefunguka mwanzo mwisho kuhusu baadhi ya wasanii kumpigia simu Director wa wimbo wa Toto kwa ajili ya kuyataka material ya wimbo huo.


(Alikiba Na Muongozaji wa Video Kelvin Bosco JNR)
Kiba amesema hayo wakati anafanya mahojiano na katika kipindi cha Playlist kinachoruka Timesfm baada ya kuulizwa, kuwa kuna baadhi ya wasanii walisemekana kumpigia simu director wa Toto ni kweli?
Alikiba alijibu ” Ni kweli kuna watu walimpigia simu Director ni kitu cha ajabu sana na sikufurahishwa nacho, kwanza sio mara ya kwanza kuna director niliwahi kugombana nae na tukaacha kufanya kazi naye kisa aliwapa watu fulani material ya wimbo wangu”

Alikiba aliongeza ” Wanachukua nyimbo zangu wanasikiliza sijui wanataka nini na najua kuna sehemu fulani wamechukua wimbo wangu fulani na hiki kitu kinaniumiza sana sipendezwi nacho kabisa, nampongeza sana Manwalter kwani hajawahi kumpa mtu yoyote wimbo wa mtu mwingine aisikilize yuko profesional sana, kwani hawezi kutoa material ya mtu hata umpe nini”.