Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Umeme Wilaya ya Kyela Kero kwa Wananchi

Tatizo la Kukatika Umeme mara kwa mara Wilaya ya Kyela Imekuwa kero kwasasa kwa Wananchi waishio ndani ya Wilaya Hiyo.

Hii inatokana na Kukatika kwa Umeme muda wowote pasipo kuwa na Sababu Maalumu.Tarehe 10/06/2018 Umeme ulikatwa Wilaya Nzima Ya Kyela Kwa Ajili ya Marekebisho ila Usiku wa Kuamkia tarehe Kumi na 13/06/2018 Umeme ulikatika kuanzia Saa 23:40 Usiku Na Umerudi Saa 07:57 Asubuhi.

Hivyo wananchi kushindwa kumudu majukumu yao kutokana na kero hiyo maana kwa Jeografia ya Wilaya ya Kyela Shughuli nyingi za kiuchumi na Maendeleo zinategemea sana Umeme.

Mwabusila Blog Inapenda kuibua Changamoto hii na Kuifikisha kwa Viongozi husika wa Tasisi hiyo kupitia Mtandao wake wa Kijamii kulingana na Kuwepo na ugumu mkubwa wa Kuwafikia Viongozi hao.

Ila bado tunajitahidi kulingana na uwezo wetu tumpate japo Manager wa Tanesco wilaya Ya Kyela Aweze  kutupa waalau Sababu ni Nini kinapelekea  tatizo la Kukatika Kwa Umeme Mara kwa Mara.

Endelea kutembelea Blogu yetu kwa Muendelezo pale tu tutapokuwa tumefanikiwa Kumpata Manager huyo au Mtendaji yoyote Katika Tasisi hiyo Ndani ya Wilaya ya Kyela