Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Tukubali mwaka huu tuliteleza -Ahmed

 


“Tukubali kiroho safi kwamba mwaka huu tuliteleza, tukishafungua nafsi maana yake kila Mwanasimba tarehe 14 atakuja uwanjani kiroho safi,” anasema Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally.

Ahmed ametoa kauli hiyo leo kuelekea mchezo wa mwisho Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien utakaopigwa uwanja wa Mkapa Jumamosi.

“Msimu huu hatujapata ushindi wowote kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika Ligi. Matokeo haya yamefanya imani imewapotea wanasimba ya kupata ushindi kwenye uwanja huo sasa tunakwenda kufuta hii dhana,” amesema Ahmed.

Ahmed amesema Simba SC hawapo tayari kupoteza mara mbili dhidi ya Stade Malien.

“Tumewahi kufungwa na wengine kama Al Ahly lakini walipokuja Kwa Mkapa tuliwarudishia. Hii ndio falsafa ya Simba. Kama ilivyokuwa kwa Petro ndio itakuwa kwa hawa wengine. Halitakaa itokee Simba tukapoteza mechi mbili dhidi ya mpinzani mmoja,” ameongeza Ahmed.