Header Ads

PropellerAds

Breaking News

“ Kigoma miradi ya barabara izingatie vipaumbele Dira 20250”

 

KIGOMA: MKUU wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro amezitaka Wakala wa Barabara (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuekeleza majukumu yao ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kuzingatia mpango wa maendeleo ya taifa na vipaumbele vya hali halisi ya mkoa Kigoma,

Balozi Sirro alisema hayo akifungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Kigoma na kubainisha kuwa mpango wa maendeleo ya taifa umeanisha kila jambo ambalo linapaswa kufanywa na taasisi na mamlaka mbalimbali za serikali na wadau wake akitaka pia vipaumbele viwekwe kwenye utekelelzaji wa miradi ya miradi ya barabara ngazi ya mkoa.

Wajumbe wa bodi ya barabara Mkoa Kigoma wakiwa kwenye kikao

Katika kikao hicho Mkuu huyo wa mkoa alizitaka mamlaka hizo za barabara kuweka kipaumbele katika utekelezaji wa barabara za mkoa huo kuendana na mpango wa serikali wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati kiuchumi na biashara kwa ajili ya nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Aidha, Balozi Sirro amezitaka TARURA na TANROADS kuongeza ubunifu katika kutafuta suluhu endelevu ya miradi ya barabara ikiwemo kuongeza matumizi ya teknolojia na gharama nafuu za miradi yaa barabara huku akitaka pia kufanyika ukaguzi wa mara kwa mara wa barabara za mkoa huo.


Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako alipongeza utekelezaji wa miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA na TANROADS lakini amebainisha kuwa bado hakuna barabara saidizi (Access Roads) wala michepuko ya barabara kuelekea maeneo ya utoaji huduma za kijamii kutoka barabara kuu.