Hivi hapa Vyuo 1000 Bora Duniani, Afrika vipo 14
June 4, 2018 Vyuo 14
tu kutoka bara la Afrika katika nchi za Afrika Kusini 7, Misri 4,
Nigeria 1, Tunisia 1 na Uganda 1 ndio vimeingia katika orodha ya vyuo
1000 bora Duniani, hili limebainishwa katika orodha ya vyuo bora Dunia
ya mwaka 2018 iliyotolewa na Center for World University Rankings(CWUR).
CWUR inapima ubora wa elimu na mafunzo
kwa wanafunzi, ufahari wa wanafunzi walio katika vitivo mbalimbali
pamoja na ubira wa tafiti bila kutegemea ‘data’ zilizokusanywa na chuo
husika.
Marekani ina jumla ya vyuo 8 katika Kumi bora, huku Chuo
Kikuu Harvard kikishika namba 1 kwa mwaka wa 7 mfululizo sasa. Chuo
hicho kinafwatiwa na Chuo Kuu cha Stanford, Chuo cha Ufundi
Massachusetts, Chuo Kikuu cha Cambridge, Chuo Kikuu Oxford, Chuo Kikuu
cha California, Berkeley, Chuo Kikuu Princeton, Chuo Kikuu Columbia,
Chuo cha ufundi California na Chuo Kikuu cha Chicago.
Katika vyuo kutoka Afrika Kusini, Chuo
Kikuu cha Cape Town kimeshika nafasi ya 223 huku ndio kikiwa Chuo cha
kwanza Afrika, kimefwatiwa na Chuo Kikuu cha Witwatersrand(230), Chuo
Kikuu cha KwaZulu-Natal(402), Chuo Kikuu cha Pretoria(438), Chuo Kikuu
Stellenbosch(448), Chuo Kikuu cha Johannesburg(790) na Chuo Kikuu
North-West(964).
Katika vyuo kutoka Misri, Chuo Kikuu
Cairo kimeshika namba 452, kikifwatiwa na Chuo Kikuu Ain Shams(715),
Chuo Kikuu Mansoura(884) na Chuo Kikuu Alexandria(903).
Chuo kutoka Uganda, Chuo Kikuu Makerere
kimeshika nafasi ya 771, Chuo Kikuu Tunis El Manar kutoka Tunisia
kimeshika nafasi ya 908 wakati Chuo cha Ibadan kutoka Nigeria kikishika
nafasi ya 991.