Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Kizungu Mkuti Uhakiki Vyeti Vya Kuzaliwa kwa Waombaji wa Mkopo Elimu ya Juu

Uhakiki wa Vyeti Vya kuzaliwa Kwa wanafunzi waombao Mkopo Kwa Mwaka Wa Masomo 2018/2019 Wameanza Kujawa na Hofu Baada Ya Mfumo huo kushindwa Kutoa Majibu ya Uhakiki ndani ya Siku Tatu Kama Ilivyo Tangazwa Na Mamlaka Husika RITA.

Mwabusila Blog Imezungumza na Mmoja wa Wanafunzi ambae ni Muhanga wa Swala Hili la Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Amesema "Nitakribani wiki ya Tatu sasa Tangu nimetuma Cheti Changu katika Uhakiki Portal ila Mpaka sasa Sijajibiwa.Napojaribu kupiga Simu inaita Lakini Haipokelewi."

Baada ya Mwabusila Blog Kupata Taarifa hii ikabidi Tupige namba hiyo lakini imeita pasipo kupokelewa na Mtoa Huduma Yoyote.Baada ya Hali hiyo tumejaribu Kuzungukia Baadhi ya Internet Cafe napo tumekutana na Changamoto hiyo na Wakaongeza kwamba Leo Mchana Uhakiki Portal hiyo na Tovuti yao www.rita.go.tz kiujumla Zilitoweka Hewani.

Mmoja Kati ya Wadau tulie Zungumza Nae Ambae Jina Lake hakutaka Liwekwe Wazi Ameshauri kwamba "Tunaiomba Serikari ibadili utaratibu huu wa kutumia Portal kwa Ajili ya Uhakiki na Itoe Muhuri huo wanao Tumia Kwa Kila Ofisi Zao Nchini Kote ili Kupunguza Kero na Adha kama Hii,ili Vijana wakamilishe maombi yao kwa Wakati."

Mwabuila Blog ikishirikiana na Wananchi tunaiomba Serikali Kulitazama Kwa Macho Mawili Swala Hili Ili Wanafunzi wanaotarajia Kujiunga na Vyuo Vikuu Watume Maombi yao ya Mkopo Kwa Wakati Baada ya Kutatuliwa Swala Hili.