Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Deal Almost Done: Fred kufanyiwa vipimo vya afya leo kujiunga Man UTD

Kiungo wa Shaktar Donetsk na raia wa Brazil Fred, imeripotiwa kuwa atafanyiwa vipimo leo jumatatu ili kukamilisha uhamisho wake wa kwenda kukipiga katika klabu ya Manchester United.

Kiungo huyo ambaye aliingia dakika ya 82 katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya taifa ya Brazil na Croatia na kushinda 2-0, anasemekana kuwa ndiye atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Mourinho katika majira ya joto.

Baada ya kushinda mchezo huo kocha wa Brazil Tite amesema kuwa, hashangai kuona Manchester United wameonesha nia ya kutaka huduma ya mchezaji huyo kwani hata yeye angekuwa meneja wa Mashetani hao wekundu angehitaji pia huduma ya Fred na amewataka kuharakisha zoezi hilo ili Fred ahamishie akili yake yote katika timu ya taifa.

Brazili watacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Austria katika jiji la Vienna June 10 kabla ya kuelekea nchini Urusi kuwavaa Uswisi, Costa Rica na Serbia katika kundi E katika mahindano ya kombe la dunia.