Ushauri wa Wataalam kuhusu Mchanga wa madini
Chama cha ACT Wazalendo
kilifanya Kongamano kuhusu Rasilimali Madini ambalo lilifanyika katika
Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa DSM kujadili masuala yanayohusu madini
likiwemo Mchanga wa Madini uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi ambao sasa
umezuiwa.
Wataalam mbalimbali wa masuala ya madini na wafanyakazi wa migodini
walikuwa ni miongoni mwa walipata nafasi ya kuchangia hoja katika
Kongamano hilo ambapo mmoja kati yao ni Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafanyakazi Migodini Nicomeds Kajungu.
“Baada ya kuwa tumesikia
kwamba kuna katazo la Serikali kwamba makenikia au mashobo
yasisafirishwe tena, sisi kama Wafanyakazi tuiona ni muhimu sana kwa
sababu ni wadau wakubwa sana…” – Nicomedes Kajungu.
Unaweza kutazama kwa kuplay VIDEO
hii ambayo ina kila kitu kuhusu ushauri wa wataalam wa Madini ambao
wameshauri nini kifanyike juu ya Mchanga wenye Madini uliozuiwa kwenda
nje ya nchi…