Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Mchezaji wa zamani wa Newcastle afariki baada ya kuanguka mazoezini

June 5, 2017 zipo taarifa mbaya zimeanza kusambaa kwenye mitandano ambazo zinaeleza kuwa kiungo wa zamani wa Newcastle United Cheick Tiote amefariki baada ya kuanguka uwanjani akiwa kwenye mazoezi China.
Tiote kiungo wa timu ya Taifa la Ivory Coast alicheza miaka saba akiwa Tyneside akicheza mechi 138 za Ligi Kuu ya England na alijiunga na Klabu ya Beijing Enterprises February mwaka huu na alikuwa mmoja wa kikosi cha Ivory Coast kilichotwaa Ubingwa wa Africa Cup of Nations 2015.
Klabu yake ya zamani ya Newcastle iliandika kwenye account ya klabu ikionesha kusikitishwa na kifo cha Tiote: “Tunasikitika kupokea kifo cha kiungo wa zamani wa Newcastle United Cheick Tioté China leo.