VIDEO: Kivuko Kipya kilichozinduliwa leo DSM
Good news kwa wakazi wa DSM hasa waishio Kigamboni leo June 5, 2017,
ni kuhusu kivuko kipya ambacho kimekabidhiwa na kitatoa huduma katika
eneo la Magogoni/Kigamboni sambamba na vivuko vya MV. Magogoni na MV. Kigamboni.
Unaambiwa kivuko cha MV Kazi kitakuwa kinatumia
dakika mbili kuvusha watu ambapo kina uwezo wa kuchukua abiria 800 na
magari madogo 22 ambapo kimetumia Tsh 7.3bn katika utengenezaji wake
kikiwekwa pia kifaa maalum chenye uwezo wa kutambua kina cha maji.
Unaweza kubonyeza play hapa chini kutazama!!!