USAJIRI BALANI ULAYA NA DILI ZILIZO KAMILIKA
MAN UTD TO YAFUFUA UPYA NIA YA KUMSAJILI GRIEZMANN
Manchester United huenda wakafufua upya lengo lao kumsajili mshambuliaji
wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, klabu hiyo ikiwa inahaha kuipata
saini ya Alvaro Morata wa Real Madrid pia, kwa mujibu wa Metro
ARSENAL YAKUBALI OFA ZA OSPINA
Fenerbahce wamefikia makubaliano na Arsenal kwa ajili ya kipa David Ospina, kwa mujibu wa Fanatik .Kipa huyo wa kimataifa wa Colombia atauzwa kwa paundi milioni 3 na
atapaa hadi Uturuki kukamilisha vipimo vya afya na kusaini dili la miaka
minne.
RONALDO KUTIMKIA CHINA KWA €200M
Cristiano Ronaldo anaweza kutolewa dau la euro milioni 200 na klabu
moja inayoshiriki Ligi Kuu ya China, kwa mujibu wa ripoti kutoka AS .
Mreno huyo amekuwa gumzo katika tetesi zilizomhusisha na klabu za
China, ingawa alitupilia mbali tetesi hizo akisisitiza anataka kubaki
Real Madrid.Sasa, Licha ya kuwa na mkataba na Real hadi 2021, inaaminika Ronaldo
amepokea ofa ya euro milioni 200 na atalipwa euro milioni 120 kwa mwaka
katika ujira wake.
PSG YAONGOZA MBIO ZA KUMSAJILI JAMES
PSG inaongoza katika mbio za kumsajili James Rodriguez wa Real Madrid, kwa mujibu wa France Football .
Mchezaji huyo raia wa Colombia anatafuta klabu itakayompa muda wa
kutosha kucheza, klabu kubwa kama Manchester United, Arsenal na Chelsea
zinaitamani saini yake lakini miamba hao wa Ufaransa wanaelekea kushinda
mbio hizo za kumsajili.