Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Habari za Uhamisho: Pata tetesi kutoka Man United, Arsenal, Chelsea, Liverpool, Barca, Madrid n.k

LIVERPOOL YAWASILIANA NA MBAPPE

 
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amewasiliana na mawakala wa Kylian Mbappe, Wekundu hao wa Anfield wakimtengea Mfaransa huyo paundi milioni 100 kwa mujibu wa  the Daily Mail .
Real Madrid wanaaminika kuwa mstari wa mbele kumwania mchezaji huyo sambamba na Arsenal, Manchester City na Manchester United.

GRIEZMANN AONGEZA MKATABA ATLETICO


Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Hispania hadi 2022, kwa mujibu wa Marca .
Mustakabali wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ulikuwa gumzo katika tetesi za vichwa vya habari akihusishwa na tetesi za kutua Manchester United.

RENATO AITOSA MAN UTD

 
Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches ataitosa Manchester United ili aweze kujiunga na Barcelona, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, 19, aling'ara katika michuano iliyopita ya Euro 2016 na akajiunga na Bayern Munichi aktokea Benfica.
Hata hivyo Sanches atauzwa baada ya kushindwa kuonyesha kandanda safi Bundesliga kwenye kikosi cha Bayern Munich. 

BARCA KUMLIPIA €80M VERRATTI

 
Marco Verratti ameomba kuondoka Paris Saint-Germain, baada ya kumwambia mkurugenzi wake mpya Antero Henrique kwamba hana raha kubaki tena Parc des Princes, L'Equipe  limeripoti.
Barcelona na Bayern Munich, ambako Carlo Ancelotti ni shabiki mkubwa wa Muitaliano huyo zipo tayari kutoa euro milioni 80 kuipata saini yake.

 CHELSEA YAMUWINDA INSIGNE

 
Chelsea wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Lorenzo Insigne wanapojiandaa kwa maisha bila ya Eden Hazard, kwa mujibu wa The Sun .
Real Madrid wapo mbioni kutoa dau nono kwa ajili ya Hazard, na Antonio Conte anataka kupata mbadala wake haraka kuepuka usumbufu majira ya joto.