TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA
BAYERN KUMLIPA ALEXIS €480K KWA WIKI
Bayern Munich wapo tayari kumfanya Alexis Sanchez kuwa mchezaji
anayelipwa zaidi, na watamlipa euro 480,000 kwa wiki, kimeripoti Kicker .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile anataka kuondoka Arsenal, na
Bayern na Manchester United zinaitaka huduma yake, lakini miamba wa
Bundesliga wapo katika nafasi nzuri zaidi kumsajili.
UNITED YAONGEZA OFA YA MORATA
Manchester United wameongeza ofa yao kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata hadi paundi milioni 60, kwa mujibu wa The Guardian .
Mashetani Wekundu walishuhudia ofa yao ya awali ya paundi milioni 52 ikitoswa na miamba hao wa Hispania.
MADRID HAWATAMNUNUA DE GEA
Real Madrid wameamua kuachana na kipa wa Manchester United David De Gea, kwa mujibu wa Marca .
CHELSEA KUMLIPA LUKAKU ZAIDI YA COSTA
Chelsea wapo tayari kumlipa Romelu Lukaku mshahara mnono kuliko Diego
Costa ili waweze kumsajili tena mshambuliaji huyo mahiri wa Everton,
kimeripoti Liverpool Echo .
Costa amedai kuwa hatakiwi tena na Antonio Conte na bosi huyo wa Chelsea anamtaka Lukaku kama mbadala wake.