Header Ads

PropellerAds

Breaking News

DAVID DE GEA KUIKOSA FAINALI YA EUROPA DHIDI AJAX HIZI HAPA SABABU

ose Mourinho amesema Sergio Romero atacheza mechi ya fainali Ligi ya Uropa dhidi ya Ajax, na David de Gea amekubali kwa furaha! Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kuwa amepanga kumwanzisha Sergio Romero langoni katika fainali ya Ligi ya Uropa dhidi ya Ajax baadaye mwezi huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina amecheza mechi 11 katika mechi 14 za Mashetani Wekundu kwenye michuano ya Ulaya msimu huu, ikiwa ni pamoja na mechi zote mbili hatua ya nusu fainali dhidi ya Celta Vigo. Akiwa pia ameanza mechi sita hatua ya mtoano, Mourinho haoni sababu ya kubadilisha kipa katika fainali hizo zitakazopigwa Stockholm Mei 24, ikimaanisha kuwa David De Gea ataangalia mpira akiwa benchi.
"Hakuna utata. Ni makipa wawili wenye uwezo mkubwa," Mourinho alisema. "Sijawahi kuona katika kipindi changu chote cha soka, makipa wawili ambao ni marafiki kama hawa, kwa sababu ni nafasi ambayo mara nyingi huwa na ushindani, hasa wote wanapokuwa katika viwango vinavyofanana. "Tunamzungumzia kipa wa taifa la Argentina na kipa wa Hispania lakini ni marafiki na wanashirikiana kwa pamoja muda wote. Sijawahi kuona sura ya huzuni baina yao. Nimewaona tu wakishirikiana muda wote. "Nadhani ni haki Sergio akicheza fainali na David amekubali hilo, hasa kwa sababu David amecheza mechi tatu za Ligi ya Uropa tayari - mbili dhidi ya Fenerbahce na moja dhidi ya Feyenoord - na hivyo kama tutashinda taji, David atakuwa mshindi wa taji pia. Kama kila kitu kitaenda sawa, hatutapata taabu yoyote, Sergio atacheza mechi ya fainali." Romero amecheza mara 26 United kwenye michuano yote tangu alipotua Old Trafford akitokea Sampdoria 2015, zaidi ya nusu ya mechi hizo zikiwa ni michuano ya Ulaya.