Header Ads

PropellerAds

Breaking News

MANCHESTER UNITED KUVUNJA REKODI YA DUNIA KWA NEYMAR JR

Klabu ya Manchester United inaripotiwa kujiandaa kuwabomoa vigogo wa Hispania, Barcelona kwa kumnyakua mshanbuliaji Neymar Jr. Kwa mujibu wa jarida la Hispania, Sport mkataba wa Neymar una kipengele cha kuuzwa kwa angalau euro milioni 200 dau ambalo Manchester United wako tayari kulilipa.
Neymar Jr Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa Brazil
Dau hilo litavunja rekodi ya dunia inayoshikiliwa na dau la euro milioni 100 alilonunuliwa Paul Pogba kutoka Juventus Julai mwaka jana. Taarifa zaidi zinasema Manchester United wako tayari kumfanya Neymar kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwa kumpa mshahara wa zaidi ya pauni 415,000 kwa wiki.