Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini ang'atuka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali na kuridhia ombi la kusitisha mkataba na kustaafu kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) John Casmir Minja.
CGP John Casmir Minja.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Minja anastaafu kuanzia leo tarehe 02 Desemba, 2016. Rais Magufuli amempongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu John Casmir Minja kwa utumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu. Wakati huo huo, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Magereza (CP) Dkt. Juma A. Malewa kuwa Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini hadi hapo uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza utakapofanyika.