Header Ads

PropellerAds

Breaking News

JINSI YA KUTUMA FILES, DOCUMENTS, PROGRAMS KWA WHATSAPP

Hello karibu katika darasa huru, asante kwa kutembelea blog yetu. Asante kwa mnaoendelea kutuma maswali yenu, kiukweli tunapokea maswali mengi sana kwahiyo ukiona swali lako halijajibiwa usidhani tumelidharau au tumelisahau, tunaendelea kuyafanyia kazi na mtapata majibu hapahapa darasani. Pia kama una swali maoni au ushauri nitumie kwa email yangu:obbymjuzi@gmail.com. Leo katika DARASA HURU tutajifunza jinsi ya kutuma mafile au mafolder ambayo sio audio au video kwa kutumia whatsaap. Hii itakuwa msaada kwa wale miokuwa mnatamani kutumiana softwares au notes au documents mbalimbali kwa njia ya whatsaap. KARIBU Whatsapp ni app ambayo imekuwa ikitumika na watu wengi kweny kutuma na kupokea audio na video, ni app inayopendwa na watu wengi sana kutokana na urahisi wake wa kutumia. Pamoja na kukuwezesha kushare files za multimedia(music, photos, video) lakini kuna kasoro iliyopo katika app hii. Nayo ni kwamba Haina uwezo wa kutuma files zilizopo katika mfumo wa software kama .exe, .apk, .bar n.k na pia files katika mfumo wa document (.docx, .pptx, .epub). Zipo njia baadhi zinazokuwezesha kutuma na kupokea mafaili ya mfumo huo, moja ya njia ambayo nadhani inafaa zaidi ni kwa kutumia programu ya kando(third party app) inayoitwa WhatsApp File Sender. Kupitia WhatsApp File Sender unaweza kutuma mafaili kama hati za kiofisi(office documents) (.doc, .docx, pptx), pdf, .epub na kadhalika. Si hayo tu, kwa kifupi unaweza kutuma na kupokea kila aina ya faili kwa WhatsApp kupitia programu hii, hata programu kama .exe (executable), .zip na .apk au chochote kile unachotaka. JINSI YA KUTUMA FILES STEPS. 1.Nenda kweny playstore na udownload Whatsapp File Sender 2. Fungua WhatsApp File Sender, kisha angalia sehem wameandika SELECT FILE au chagua mafile utakayayaona chini ya hio neon SELECT FILE. 3. Tafuta faili unalotaka kutuma, kisha SEND 4. itakupeleka kwenye whatsapp account yako 5. Chagua unaemtumia kisha bonyeza "OK". NAMNA YA KUPOKEA FAILI STEPS 1. Download faili kwa WhatsApp yako ya kawaida 2. Baada tu ya kudownload, WhatsApp File Sender itafunguka yenyewe na kuomba ruhusa yako ili kufungua faili hilo (decode). 3. Elekeza sehemu unayotaka kuhifadhi hilo faili, unaweza tengeneza folder lake maalum kwa ajli tu ya kupokea mafaili kwa njia hii. 4. Kisha bonyeza Ok. NOTE Ili kufanikisha swala hili ni Lazima wote (mtumaji & mpokeaji ) wawe na WHATSAPP FILE SENDER (WTS) WhatsApp File Sender hubadili mafaili (encoding) kwenda kwenye mfumo wa sauti (audio), na wakati wa kupokea hurudisha katika mfumo wake wa kawaida (decoding). Kwa Kawaida WhatsApp hutuma faili lisilozidi ukubwa wa MB 16, lakini kwa njia hii unaweza kutuma faili lenye ukubwa wowote zaidi ya MB16. Unaweza tuma vitu vingi kwa mara moja, tengeneza folder la ".zip" weka mafaili yote ndani yake, kisha tuma. WhatsApp File Sender hugawa mafaili makubwa katika ukubwa wa MB 16 kila moja, hii huwezesha kutuma mafaili makubwa zaidi. Mpokeaji ni lazima ahakikishe vipande vyote vimefanikiwa kuwa downloaded kabla ya decoding. Hii ni Njia nzuri kwa makundi ya WhatsApp kutumiana mafaili ya kiofisi kama notes na mengineyo kwa urahisi zaidi.