Header Ads

PropellerAds

Breaking News

ZITTO KABWE AFUNGUKA MAMBO MAZITO,ASEMA TUSIKUBALI KUIBIWA TENA.

Zitto Kabwe Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo azungumza haya Leo huko Masasi,Mtwara. Ufisadi wa $600m hati fungani za Serikali: Tusikubali ya Rada, hatua zichukuliwe Taasisi ya Serious Fraud Office ya Uingereza ( SFO ) inafanya mazungumzo na Benki ya Standard Group ya Afrika ya Kusini Lakini iliyoorodheshwa katika soko la hisa ya Uingereza ( London Stock Exchange ) ili kumalizana kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa hati fungani za Serikali ya Tanzania yenye thamani ya dola za kimarekani milioni Mia Sita ( $ 600m ). Mazungumzo hayo yanafanywa mbele ya Jaji katika mji wa London. Ndugu wanahabari, ni jambo la kawaida kwa serikali yoyote duniani kuuza hati fungani. Mnamo mwaka 2011/2012 Serikali kupitia Wizara ya Fedha iliuza hati fungani ( Bonds ) zenye thamani ya dola za kimarekani 600 milioni ($600 million), dhamana hizo za serikali zilinunuliwa na benki ya kigeni (Stanbic) ambayo ni mali ya Standard Group ya Afrika ya Kusini, yenye makao makuu yake huko London, Uingereza. Hata hivyo, sehemu ya fedha hizo haikuingia kwenye akaunti za Serikali ya Tanzania na pia gharama za Bond hiyo zilipaishwa kupitia wakala wa kati kati ( middle men ) na hivyo kupelekea rushwa ya takribani $60 milioni kutolewa Kwa maafisa waliothibitisha biashara hiyo. Ndugu wanahabari, taasisi za kiuchuanguzi za nchini Uingereza, hasa ile ya kushughulikia makosa ya rushwa (Serious Fraud Office-SFO) tayari imeshafanya uchunguzi wake wa awali kwa kuhusisha pande zote.