VIDEO: A-Z Mnyika alivyotolewa nje ya Bunge na Askari
Moja ya stori kubwa kutokea Bungeni Dodoma leo June 2, 2017 ambayo
ina-make headline ni Wabunge wa Upinzani kususia Vikao vya Bunge hatua
iliyokuja baada ya agizo la Spika Job Ndugai kumsimamisha Mbunge wa
Kibamba John Mnyika kutoshiriki Vikao vya Bunge kwa muda wa wiki moja
kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha mbele ya Bunge na kuwaagiza
Polisi kumtoa nje.