TETESI ZA USAJIRI MAJUU:MAN UTD YATAKIWA KUTOA £50M KUMSAJILI DIER
Manchester United wameambiwa watoe paundi milioni 50 au zaidi kumsajili kiungo wa Tottenham Eric Dier, Telegraph limeripoti.
Jose Mourinho anataka mchezaji huyo wa Spurs asajiliwe kabla ya msimu
mpya kuanza, lengo ni kutafuta mrithi wa kudumu wa Michael Carrick.
MENDES AIAMBIA REAL RONALDO ANA OFA KUTOKA UINGEREZA
Wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes ameiambia Real Madrid kuwa
mshambuliaji huyo amepokea ofa kadhaa kutoka klabu za Ligi ya Uingereza,
kwa mujibu wa Cope
MAN UTD & JUVE ZAMFUATILIA GOMES
Manchester United na Juventus zinafuatilia maendeleo ya kiungo wa Barcelona Andre Gomes, kwa mujibu wa habari za AS .
Gomes amekuwa na mwanzo mgumu Barcelona na Mreno huyo anaweza
kutimkia kwenye klabu mojawapo kati ya Juventus na Manchester United.