Izzo Bizness asema hategemei show za Dar
Msanii kutoka 'Green City' akiwakilisha kundi la The Amaizing, Izzo
Bizness amedai hawezi kulala njaa kusubiri simu za promota kwa ajili ya
show kwani kipaji anacho ndio maana anajiongeza zaidi mikoani.
Izzo amefunguka hayo baada ya maswali mengi kuzuka kwa nini hana 'show'
nyingi Dar Es salaam kama mikoani, na kueleza kwamba muziki ni biashara
yake hivyo hataweza kubweteka huku biashara yake inaharibika..
"Sikai kutegemea mpaka Promota anipigie simu kuhusu show maana hapo kuna
kuna kuanza mazungumzo na kushushana bei, ila natengeneza mwenyewe
najijua mikoa flani ndani ya Tanzania nakubalika nachukua opportunity
hiyo kutengeneza show hizo peke yangu na mwisho wa siku maisha
yanaendelea. Haipendezi msanii kama mimi nianze kupiga vizinga hadi vya
vocha , Hata prof. Jay aliwahi kusema kama kipaji unacho kwa nini ufe na
njaa, na ndivyo nifanyavyo mimi ", Izzo alifafanua
Aidha Izzo ameongeza kwamba pamoja na changamoto kama kundi la The
Amaizing wanazokumbana nazo amewataka wasanii waimbaji wajipange sana
kwani ujio wa Abella Music lazima uwatingishe kwenye game.
"Kwa sasa The Amaizing tuna changamoto ukizingatia Abella ni mgeni ndo
anaanza kutengeneza mashabiki kwa hiyo na uhakika akishapata kile
anachohitaji atakuwa moto balaa na nitoe angalizo kwa waimbaji siyo kwa
kuwa-disrespect hapana ila ujio wa Abella lazima uwasumbue hivyo
wajipnge sana", Izzo aliongeza.