FAIDA 6 ZA KUWA NA WEBSITE KWA AJILI YA BIASHARA AU NGO
Je umekua ukisikia tuu swala la kuwa na website lakini
hujaelewa kwanini haswa uwe na website kwa ajili ya biashara au asasi yako
isiyo ya kiserikali (NGO)? Au unayo website lakini haujaona bado faida za kuwa
na website ? Basi makala hii itakupasha
faida haswa ya kuwa na website kwa namna ambayo pengine hujawahi
kufikiria.
Hakuna wakati ambao website ni ya muhimu kama wakati ambapo tupo katika zama za utandawazi. Yawezekana ukajiona kuwa unachofanya ni kidogo hivyo hauhitaji website , hata hivyo kuna mengi utakua unakosa kwa kutokujikita katika kuwa na website kwa biashara au asasi yako.

Kukipa thamani
ufanyacho
Imekua kawaida watu wengi kuamini kuwa biashara au asasi yenye website basi itakua makini . Hata hivyo sio tuu website ili mradi website. Unatakiwa uwe na website ambayo kweli inaonyesha umakini na ubora wa asasi au biashara yako hii inajumuisha website yenye muonekano mzuri, yenye maelezo yaliyokamilika, yenye taarifa ambazo kweli.

Kuleta ushawishi
Unahitaji website ili kuweza kujenga uaminifu na kuonekana
kweli upo serious. Website yako itakupa nafasi ya kuwaeleza watu kwa umakini na
kwa ushawishi kile unachofanya na
kwanini wakutafute wewe. Tena website itakusaidia kufanya ushawishi huu kwa
watu wengi sana kuliko kuwa tuu na vipeperushi ambavyo utasambaza kwa watu
wachache.
Kuelezea Ufanyacho
Website hukufanya uwe na nafasi ya kueleza mambo uyafanyacho
kwa watu wengi zaidi. Ni kweli unaweza kuwa na akaunti nyingi za mitandao ya
kijamii . Lakini watu wengi hawatopata kukufahamu vizuri kama sio kupitia kwa
website yako ambapo utakua na kurasa zilizopangiliwa vema kabisa.
Kupatikana wakati masaa
24 siku 7 za wiki
Ofisi yako hufungwa , duka lako hufungwa, lakini website yaweza kupatikana masaa 24 siku 7 za wiki. Hivyo kuwa na website ni fursa kwako kuwafaikia walengwa wako masaa yote kila siku.
Ofisi yako hufungwa , duka lako hufungwa, lakini website yaweza kupatikana masaa 24 siku 7 za wiki. Hivyo kuwa na website ni fursa kwako kuwafaikia walengwa wako masaa yote kila siku.
Kuwasiliana na
kuwaelimisha wateja
Kwa kutumia blog itakayoambatana na website yako utaweza
kuwapatia wateja wako na wale wateja watarajiwa Makala ambazo zitawaelimisha na
kuwavuta karibu na wewe. Pia ni nafasi yako ya kuwapa updates kuhusu bidhaa
mpya unazotaka kutoa au mabadiliko mengine ya kiutendaji , kimarketing na sera
za biashara au asasi yako.
Kuwa na email address
binafsiWebsite itakufanya uweze kuwa na email address inayotaja jina la biashara yako. Haipendezi na haionekani kuwa “professional” pale unapohitajika kutaja email address yako halafu ukatumia email yenye domain ya makampuni makubwa kama gmail, yahoo au Hotmail. Kama kampuni yako ni ABC Limited, basi ni vema ukasema jinalako@abc.com au jinalako@abc.co.tz (chanzo cha makala http://mbuke.blogspot.com.)
Kama unahitaji kuwa na website yako binafsi tuwasiliane kwa namba +255 744 195 910