Header Ads

PropellerAds

Breaking News

NYOKA ASABABISHA EMIRATES KUAHIRISHA SAFARI YA NDEGE

Safari ya ndege ya Shirika la Emirates ya kutoka Oman kwenda Dubai imesitishwa baada ya wahudumu wa ndege hiyo kukuta nyoka ndani ya ndege.Safari ya ndege nambari EK0863 kutoka Muscat ilisitishwa baada ya wafanyakazi wa kupakia mizigo kugundua kuwa kulikuwa na nyoka kwenye eneo la kubebea mizigo.
Msemaji wa shirika hilo amenukuliwa na vyombo vya habari Dubai akisema nyoka huyo aligunduliwa kabla ya abiria kupanda ndege hiyo. Ndege hiyo ilichunguzwa kwa makini kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari na muda mfupi baadaye iliwasili Dubai. Emirates hawakusema ni nyoka wa aina gani aliyepatikana kwenye ndege au iwapo ni nyoka hatari au la!.Wengi wamefananisha kisa hicho na filamu ya Samuel L Jackson ya mwaka 2006 kwa jina Snakes on a Plane (Nyoka kwenye Ndege) ambapo abiria wanakumbana na mamia ya nyoka wadogo wenye sumu ndege ikiwa katikati ya safari. Baadhi ya watu wameanza kujadili filamu hiyo mitandao ya kijamii. Hii si mara ya kwanza kwa nyoka kugunduliwa kwenye ndege, hasa maeneo yenye joto.Novemba mwaka jana, nyoka wa urefu wa mita tatu aligunduliwa kwenye ndege Mexico. Chatu mwingine alionekana akining’inia kwenye ubawa wa ndege iliyokuwa safarini kutoka Cairns, Australia hadi Port Moresby nchini Papua New Guinea mwaka 2013. Na mwaka 2012, maafisa wa kuwahudumia wanyama walimuokoa nyoka mdogo aliyegunduliwa kwenye ndege iliyowasili Scotland kutoka Mexico.