Header Ads

PropellerAds

Breaking News

Imethibitishwa Squid Game Season 2 inakuja

 


Baaada kufanya vizuri kwa series ya Squid Games msimu wa kwanza kupitia jukwaa la Netflix na mahitaji ya muendelezo wake yakiwa mkubwa kwa mashabiki, hatimaye mwandishi na muongozaji wa series hiyo Hwang Dong-Hyuk amethibitisha kuwa msimu wa pili unakuja.

Hwang Dong-Hyuk amethibitisha hilo kupitia mahojiano na Associated Press ambapo amesema wamefikia uamuzi huo kuuleta muendelezo wake kutokana na uhitaji makubwa ya watu.

“Nachoweza kusema ni kwamba sehemu ya pili itakuwepo, ipo kichwani mwangu sasa hivi. Kumekuwa na msukumo mkubwa, uhitaji mkubwa na mapenzi makubwa ya sehemu ya pili. Kwasasa ni mapema sana kusema ni lini” –Hwang Dong-Hyuk.

Squid Game ambayo ilitoka Septemba 17, ni kati ya series zilizotoka mwaka huu na kufanya vizuri ndani ya muda mfupi.