PICHA 3: Samatta na Omar Colley wameenda hija Macca
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza club ya KRC Genk ya
Ubelgiji Mbwana Samatta wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani ameamua kwenda Saudi Arabia Macca kuhiji.
Mbwana Samatta kupitia ukurasa wake wa instagram akiwa na mchezaji
mwenzake raia wa Gambia ambao wanacheza wote katika club ya KRC Genk
Omar Colley wamepost picha wakiwa pamoja katika ibada ya umrah.
Kitendo hicho Samatta na Colley kwenda hija anaungana na mastaa wengine
wa soka dunia ambao pia wamewahi kwenda Macca kuhiji na kufanya ibada ya
umrah kama Mesut Ozil wa Arsenal na Paul Pogba wa Man United ambao nao
ni waumini wa dini ya kiislam.
Samatta na Omary Coley